1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa ugaidi Brussels afariki kwa majeraha

17 Oktoba 2023

Mtu anayeshukiwa kuhusika na mauaji ya raia wawili wa Sweden mjini Brussels amefariki kutokana na majeraha akiwa hospitalini baada ya polisi wa Ubelgiji kumpiga risasi.

https://p.dw.com/p/4XcRs
Belgien, Brüssel | Schüsse im Zentrum
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Mwanamme huyo, mwenye umri wa miaka 45 na mwenye uraia wa Tunisia, alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na polisi siku ya Jumanne (17 Oktoba) kwenye mkahawa kwa kuwauwa mashabiki wawili wa soka raia wa Sweden mjini Brussels.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ubelgiji Annelies Verlinden amethibitisha kifo chake katika taarifa aliyoiandika kwenye mitandao ya kijamii.

Soma zaidi: Brussels yatangaza tahadhari ya tishio la kigaidi

Mbali na raia hao wawili wa Sweden waliopigwa risasi na kuuliwa, mwingine wa tatu alijeruhiwa katikati mwa Brussels usiku wa Jumatatu kabla mechi ya kufuzu kwa Kombe la EURO 2024 kati ya Ubelgiji na Sweden.

Mwanamme mmoja aliyejitambulisha kama mwanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu alidai kuhusika kwenye video iliyochapishwa mtandaoni.

Timu ya taifa ya Sweden imeshaondoka Brussels baada ya mechi yao kusitishwa wakati wa kipindi cha mapumziko wakiwa sare ya 1-1.