1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Mshukiwa wa shambulio la kisu Ujerumani ajisalimisha Polisi

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Mwanamume mmoja raia wa Syria amejisalimisha na kukiri kuwauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine wanane katika shambulio la kisu kwenye tamasha la mtaani, ambalo kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika nalo.

https://p.dw.com/p/4jtZV
Solingen, Ujerumani | Polisi wakiwa katika eneo lililotokea shambulio
Polisi Ujerumani wakiwa katika eneo la lililofanyika shambulizi la kisu.Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Polisi imesema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 26 alijisalimisha kwenye mamalaka zinazosimamia uchunguzi wa mkasa huo uliowashtua wengi.

Kulingana na magazeti ya Bild na Spiegel, mshukiwa huyo aliwasili Ujerumani mnamo Desemba 2022 na alikuwa na hadhi ya mhamiaji anaelindwa, ambayo hutolewa kwa watu wanaokimbia vita nchini Syria. 

Hata hivyo mshukiwa huyo hakujulikana na idara za usalama kama mfuasi wa itikadi kali.

Aidha mwendesha mashtaka wa Duesseldorf, magharibi mwa Solingen Markus Caspers amesema kwamba, polisi inamshikilia kijana mwingine mwenye umri wa miaka 15 anaetuhumiwa kutoripoti kitendo hicho cha uhalifu.

Soma pia:Polisi ya Ujerumani yapata kifaa inachoshuku kimetumika katika shambulio la Solingen

Kulingana na madai ya mashahidi wanasema kijana huyo alionekana kuzungumzia mkasa huo.

Ujerumani imekuwa katika hali ya tahadhari kutokana na  mashambulizi ya watu wenye itikadi kali tangu vita vya Gaza vilipozuka mnamo  Oktoba 7 baada ya Hamas kuishambulia Israel.