1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Mshukiwa wa mlipuko wa gesi Nairobi apandishwa kizimbani

6 Februari 2024

Mshukiwa mkuu wa mlipuko wa gesi uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika mtaa wa Embakasi mjini Nairobi amefikishwa mahakamani leo.

https://p.dw.com/p/4c6Tf
Kenya | Mlipuko wa gesi uliotokea mjini Nairobi
Athari za mlipuko wa gesi uliotokea mjini Nairobi, Kenya mnamo Februari 2, 2024 Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Derrick Kimathi, ambaye polisi wanasema alikodisha "kwa njia haramu" sehemu ya kuhifadhi mitungi ya gesi kulikotokea mlipuko huo, alifikishwa mahakamani akiwa amevaa kofia nyeusi na barakoa usoni.

Wakili wake ameeleza kuwa, Kimathi atashirikiana na polisi lakini amekanusha kuwa, mteja wake alikuwa anasimamia sehemu hiyo ya kuhifadhi mitungi ya gesi.

Watu sita walipoteza maisha na wengine 280 walijeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi kulipuka usiku wa kuamkia Ijumaa, na kusababisha moto mkubwa katika eneo la Embakasi, kusini mashariki mwa Nairobi.

Rais William Ruto amesema kuwa leseni zilitolewa kimakosa kwa wafanyibiashara wa kuuza gesi karibu na makaazi ya watu kwa sababu ya uzembe na ufisadi.