1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa mauaji ya kupanga Rwanda awekwa rumande siku 30

27 Septemba 2023

Mahakama moja nchini Rwanda hapo jana imeamuru mshukuwa mmoja wa mauaji ya kupanga ya watu wengi abakie rumande kwa siku 30 wakati akisubiri shauri lake.

https://p.dw.com/p/4WrJB
Mabaki ya mafuvu ya binadamu
Mabaki ya mafuvu ya binadamuPicha: Vacca/Emblema/ROPI/picture alliance

Mshukiwa huyo, Denis Kazungu, mwenye umri wa miaka 34, alifunguliwa mashtaka wiki iliyopita baada ya miili kadhaa ya watu kufukuliwa kutoka katika shimo liliobainika ndani ya chumba cha jiko lake. Amefunguliwa mashtaka yanayojumuisha mauaji, ubakaji, ulaghai, na kunajisi miili ya watu waliokufa. 

Katika kikao cha wiki iliyopita, Kazungu alikiri mahakamani kuwauwa wanawake 13 na mwanaume mmoja, kwa madai kwamba walimwambukiza virusi vya ukimwi. 

Soma pia:Rwanda: Mshukiwa akiri kuwaua watu 14, waliomuambukiza VVU

Kesi hiyo imelitikisa taifa hilo la Afrika mashariki na hapo jana mamia ya watu ikiwa ni pamoja na ndugu wa wahanga walijitokeza mahakamani kwenye mji mkuu, Kigali kusikiliza uamuzi wa mahakama juu ya mtuhumiwa huyo. Waendesha mashtaka wamesema mshukiwa huyo hajaonesha majuto kwa matendo yake.