Mshauri wa Berlusconi ahukumiwa miaka 5
22 Novemba 2003Matangazo
ROMA: Mahakama mjini Milan imemhukumu kifungo cha miaka mitano aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Uitalia, Cesare Previti. Mahakama hiyo ilithibitisha kuwa Previti alikuwa na hatia ya kushiriki katika kashfa ya rushwa iliyohusishwa na Shirika la Uchapishaji, FINIVEST la Waziri Mkuu Sylvio Berlusconi. Alikutikana na hatia kwa sababu wakati alipokuwa wakili wa shirika hilo aliwalipa mrungura mahakimu ili kulinufaisha kibiashara shirika la Waziri Mkuu Berlusconi. Kwanza mwenyewe Waziri Mkuu wa Uitalia alihusishwa na kashfa hiyo, lakini alinusurika na mashtaka ya rushwa baada ya kupitishwa haraka sheria mpya inayobishwa vikali nchini.