Jeshi hilo limesema ni mapema kulihusisha tukio hilo na ugaidi na linaendelea na uchunguzi huku bado wananchi katika eneo hilo wakibaki na wasiwasi juu ya tukio.
Milio ya risasi iliosikika kwa takriban dakika arobaini picha za video zikimuonesha mwanaume mwenye miraba akitamba mbele ya nje wa ubalozi wa ufaransa ulio pembeni ya benki ya stanbick katika barabara ya kenyata na kinondoni, tukio ambalo lilisitisha kabisa shughuli za kijamii ikiwemo usafirishaji.
Jeshi la polisi limesema katika majibizano hayo polisi imefaulu kumdhibiti mtu huyo huku watu wanne wameuwawa watatu wakiwa ni askari polisi na mwingine ni mlinzi wa kampuni binafsi. Aidha, watu wengine sita wamejurihiwa vibaya na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya taifa muhimbili.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea
Liberatus Sabasi kamishna wa oparesheni na mafunzo jeshi la polisi nchini amesema ni mapema kulihusisha tukio hilo na ugaidi isipokuwa wanaendelea na uchunguzi wa kina kujua zaidi yalio nyuma ya mhalifu huyo ambae alijizatiti kwa silaha za moto.
Rais Samia kupitia mtandao wake wa twitter ameoelezea kusikitishwa na tukio hilo na ametuma salamu za pole kwa familia za marehemu na jeshi la polisi na kulielekeza uchunguzi wa kina ufanyike.
Taarifa katika mitandao ya kijamii zinadai kwamba, mshukiwa ni kijana mkazi wa eneo la upanga mjini Dar es salaam akiwa na umri wa chini ya miaka thelathini na tano, hata hivyo kamishna Liberatrus amesema, watathibithisha hayo kupitia upelelezi ambao tayari umeshaanza.
Taharuki yasababisha watu kupoteza mali
Katika barabara ambayo tukio hilo limefanyika hali imeonekana kuzorota huku baadhi ya watu ambao walikuwa wakifanyabiashara nyakati za foleni za magari na ombaomba wanasema hali ilikuwa ni taharuki kubwa na ya kuogofya. Wamepoteza kila kitu.
Mashuhuda wanadai wakati mwanamume huyo akiendelea na majibizano na askari alionekana kuwasiliana kwa simu na kutoa maelekezo.
Wachambuzi wa mambo wamelitaka jeshi la polisi kutochukulia tukio hilo la kawaida, kwani ukanda wa kusini mwa Afrika unakabiliwa na tishio kubwa la ugaidi na vikundi vya kihalifu vilivojiimarisha kwa silaha za kila namna.