Msako unaongezeka wa kumkamata Bin Laden.
29 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON: Marekani ina niya ya kuongeza operesheni zake za kumsaka mkuu wa chama cha Al Qaida, Usama Bin Laden, liliarifu gazeti la Kimarekani, NEW YORK TIMES. Rais George W. Bush amekwisha saini kibali cha kuanzishwa operesheni hiyo, liliarifu gazeti hilo katika ukurasa wake wa Internet. Operesheni hiyo ya kumsaka Bin Laden na wafuasi wake wa itikadi kali itatumia mikakati mipya, ilisemekana. Inashutumiwa kuwa Bin Laden amejificha katika lile eneo baina ya mpaka wa Pakistan na Afghanistan. - Serikali ya Marekani imekanusha ripoti ya Redio Iran kwamba Bin Laden amekwisha tiwa mbaroni kitambo sasa nchini Pakistan. Nayo serikali ya Pakistan imekanusha ripoti hiyo.