1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada zaidi watakiwa kwa kikosi cha Umoja wa Afrika Somalia

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdwA

NEW YORK

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana limetowa wito wa kutolewa michango zaidi ya fedha kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kinachokabiliwa na ukata wa fedha na kwa mara nyengine tena limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuendelea kupanga uwezekano wa kutuma kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mwezi uliopita alikataa kupelekwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia kuchukuwa nafasi ya kile cha Umoja wa Afrika kwa hoja kwamba Somalia ni mahala pa hatari mno kutuma timu ya kutathmini hali ya usalama kwa ajili ya kuwekwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

Baraza hilo pia limesema linasubiri kusikia maelezo zaidi ya mapendekezo kutoka kwa Ould-Abdalla mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia juu ya kuboresha usalama na kuendeleza usuluhishi wa kitaifa katika nchi hiyo ambayo imekuwa haina serikali madhubuti tokea mwaka 1991.