1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Msaada wa kwanza wa kiutu waingia ukanda wa Gaza

21 Oktoba 2023

Malori ya kwanza yaliobeba bidhaa za msaada yameingia Ukanda wa Gaza hii leo kupitia mpaka wa Rafah ulioko kati ya Misri na ukanda huo.

https://p.dw.com/p/4XqXz
Malori yaliobeba msaada wa kiutu yakisubiri kuvuka mpaka wa Rafah Oktoba 21,2023
Malori yaliobeba msaada wa kiutu yakisubiri kuvuka mpaka wa RafahPicha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

Ripoti za kituo cha televisheni cha al-Qahera cha Misri, zimesema kuwa malori 20 yanayobeba bidhaa za matibabu yamewasili huko Gaza. Huo ni msaada wa kwanza wa kiutu kupelekwa katika eneo hilo tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas wiki mbili zilizopita.

Soma pia: Guterres atembelea mpaka wa Rafah kuhimiza msaada kwa Gaza

Kulikuwa na miito ya Gaza kupatiwa msaada wa kiutu haraka baada ya Israel kuzuia uingizwaji wa mahitaji muhimu ikiwemo maji, chakula, madawa na nishati ya mafuta.

Israel inasema inataka kulisambaratisha kundi la Hamas

Hatua hiyo iliambatana na mashambulizi makali ya makombora ya Israel ndani ya eneo la Gaza kujibu shambulizi la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas ndani ya ardhi ya Israel. Israel inasema inataka kulisambaratisha kundi la Hamas inalolizingatia kuwa la kiagidi.