1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada wa Iran kwa Lebanon

20 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJq

TEHERAN:

Iran nayo imetangaza leo inapanga msaada mkubwa wa kujenga upya mitaa ya Lebanon ilioteketezwa katika vita.Baada ya mapatano ya kusimamisha mapigano yaliosimamiwa na Um kuanza kazi rasmi, kiongozi wa Hizbollah Sayyed Hassan Nasrallah ,aliahidi kuwapatia fedha za kutosha wakaazi wa majumba kiasi ya 15.000 yalioteketezwa nchini Lebanon.

Mkutano wa wafadhi juu ya msaada wa kibinadamu umepangwa August 31,mjini Stockholm,Sweden na mwengine utafanyika kujishughulisha moja kwa moja na kujenga upya m iundo-mbinu ya Lebanon.

Taarifa nyengine kutoka Tegheran,inasema Iran haitasimamisha mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.Msemaji wa wizara ya nje Reza Asefi amewaambia maripota kwamba, kusimamisha utaratibu huo ni sawa na kurejea katika hali ya zamani na Iran haina azma hiyo.