1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa bomu wauwa wanne Pakistan

10 Aprili 2023

Takriban watu wanne wameuawa leo hii na wengine 15 kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko wa bomu katika jimbo la kusini magharibi la Balochistan nchini Pakistan.

https://p.dw.com/p/4Psbh
Pakistan | Selbstmordattentat in Quetta
Picha: NASEER AHMED/REUTERS

Takriban watu wanne wameuawa leo hii na wengine 15 kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko wa bomu katika jimbo la kusini magharibi la Balochistan nchini Pakistan.

Bomu hilo lililenga gari ya polisi katika soko lenye shughuli nyingi huko Quetta, mji mkuu wa Balochistan, ambao ni maskani ya waasi kadhaa wanaotaka kujitenga na wenye itikadi kali.

Afisa wa polisi, Azfar Mehsar, amesema uchunguzi wa awali unaonesha mripuko umesababishwa na bomu lililotegwa kwenye pikipiki na kufyatuliwa kwa rimoti. Hakuna kundi lililokiri kuhusika na mauwaji hayo.

Kwa miaka mingi, Pakistan imekuwa ikipambana na uasi wa wanamgambo wa Balochistan ambao wanadai sehemu ya utajiri wa jimbo hilo, pamoja na mashambulizi ya kundi la Tehreek-e-Taliban Pakistan, Wataliban wa Pakistan.