Mradi wa kinu cha nyuklia wakosolewa
28 Julai 2007Matangazo
Wanasiasa wengine kutoka vyama CDU na SPD vya serikali ya mseto ya Ujerumani wamesema,hatua ya Ufaransa inachukuliwa mapema mno na huenda ukawa hatari.
Wakati huo huo, Gernot Erler wa SPD,alie waziri wa dola katika wizara ya nje ya Ujerumani amesema:
“La kuulizwa hapo,ikiwa ni busara kufanya kazi zaidi na Gaddafi,kazi hiyo inapohusika na teknolojia ya nyuklia na silaha au upo uwezekano mwingine pia.“
Siku ya Alkhamisi,Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy alitia saini taarifa ya maelewano pamoja na Libya,ikihusika na makubaliano ya kujenga kinu cha nishati ya nyuklia.
Hatua hiyo imechukuliwa miaka minne kufuatia tangazo la Rais wa Libya, Muammar Gaddafi,kufutilia mbali miradi ya nchi hiyo,kutengeneza silaha za nyuklia,kemikali na kibiolojia.