1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kuongeza vikosi vya amani kusini mwa Lebanon

Ramadhan ali19 Julai 2006

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umetuwama tena juu ya mzozo wa Mashariki ya kati na hasa pendekezo la katibu mkuu Kofi Annan Kuimarisha idadi ya vikosi vya UM viliopo huko.

https://p.dw.com/p/CHVV
Picha: AP

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung laandika kwamba kutumwa kwa vikosi vya UM kusini mwa Lebanon kwa kadiri Hizbollah haikushindwa vita bali inavurumisha makombora katika mji wa Haifa na kusherehekea ushindi au kwa kadiri Israel haikutimiza shabaha yake ya kijeshi,hizi- lasema gazeti ni pande mbili za sarafu moja.

Hadi swali hili limefafanuliwa, laandika FAZ ,kuna hatari pia ya kuzagaa vita.Kushambuliwa mji wa Tel Aviv kwa makombora,Israel huenda ikajibisha kwa hujuma dhidi ya dola ziliopo nyuma ya wafuasi wenye itikadi kali na manaidi huko Gaza na Lebanon.Hapo tena shabaha nyengine utakua mji wa Damascus.

Ama gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linalotoka Erfurt laandika:

„Uamuzi wa kutuma vikosi zaidi utakuwa na athari kubwa:Endapo kikosi cha kuhifadhi amani cha Umoja wa ulaya kikiwekwa mpakani kati ya Lebanon na Israel kumtuliza shetani, pakizuka balaa zaidi mambo yatakuwa magumu.Chama cha FATAH huko mwambao wa Gaza kimeshaonesha hamu ya mpango kama huo.Katika Umoja wa Ulaya juhudi za kidiplomasia za UM zinaangaliwa kwa jicho la kusitasita.“

Kwa maoni ya OFFENBURGER TAGBLATT vikosi vya UM vimekuwapo Lebanon tangu miaka 28 sasa .Idadi yao ni 2000.Kuongeza vikosi alfu zaidi hakutachangia amani.Kinyume chake, lasema gazeti:Hali kama nchini Irak yaweeza kuchomoza.

Kwani huko Irak,majeshi ya Marekani yaliojizatiti kisilaha yanashindwa kuweka amani na kupambana na magaidi.

Kwa maoni ya gazeti la MAINZ-ALLGEMEINEN ZEITUNG vikosi vya kuhifadhi amani hasa viwe na jukumu la kuilinda Israel.Linasema kuwa makombora yanayofika mbali ya Hizbollah yana uwezo wa kuuhujumu hata mji wa Tel Aviv.

Isitoshe, spika wa bunge la Iran amesema mwanzo wa kuiteketeza dola ya wayahudi umewadia.Ikiwa ndio hivyo, lasema gazeti, Israel inahitaji msaada mkubwa na mashariki ya kati kuwa na kikosi cha kuhifadhi amani ambacho kitaweza kuzima hujuma za makombora ya Hizbollah.

Ikiwa si hivyo mnamo muda mfupi,kutatokota balaa ambalo sio tu litaishia Mashariki ya kati.

Likitumalizia uchambuzi juu ya mada hii, gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG laandika kuwa, kuna shaka shaka iwapo kuongeza vikosi vya kuhifadshi amani vya UM kutachangia kweli kuleta amani….

Kwa kadiri UM ,Umoja wa Ulaya na kundi la dola kuu 8 tajiri-G-8, kutokana na masilahi mbali mbali tangu ya kisiasa hata ya kiuchuimi zitakwepa kuwawekea mpaka wa kibalozi waliozusha balaa hili,basi mauaji yataendelea.

Iran laongeza gazeti, imeelewa kugeuza macho ya walimwengu upande mwengine wa mgogoro wake wa mradi wa nuklia.Kwa upande mwengine,balaa hili la umwagaji damu linadhihirisha wazi hatari ya kuripuka pipa la baruti endapo Iran ikija kuwa dola la kinuklia.