1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moyo: Mansoor hakutendewa haki

22 Agosti 2013

Kamati Maalum ya CCM Zanzibar ilipitisha azimio la kumvua uwanachama wa chama hicho Mansoor Yussuf Himid, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kiembesamaki, waziri wa zamani na mjumbe wa Kamati ya Maridhiano.

https://p.dw.com/p/19UlA
Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ali Mohamed Shein.Picha: DW

Inatarajiwa kwamba hapo kesho Ijumaa, Kamati Kuu ya CCM itakutana mjini Dodoma, ambapo moja ya ajenda zake ni suala hili la kufukuzwa kwa Mansoor kwa sababu ya kuunga kwake mkono madai ya muundo wa Muungano wa Mkataba, ambayo ni kinyume na sera ya Muungano wa Serikali Mbili inayofuatwa na CCM.

Mohammed Khelef amezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano visiwani Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo, ambaye kama alivyo Mansoor, naye ni mwanachama wa CCM na mtetezi wa muundo wa Muungano wa Mkataba, na kwanza alimuuliza ameupokeaje uamuzi huu.

Kusikiliza mahojiano hayo kwa ukamilifu, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Khelef/Moyo
Mhariri: Josephat Charo