1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urusi yasihi Marekani kusimamisha mpango wa kuweka makombora Poland

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBph

Mkuu wa majeshi ya Urusi anatoa wito kwa Marekani kusimamisha kwa muda hatua za kuweka makombora ya kujihami nchini Poland na Jamhuri ya Czech.Kwa mujibu wa Jenerali Yury Baluyevsky aliyezungumza na waandishi wa habari radar ya nchi yake iliyo nchini Azerbaijan iliyopendekeza kutumiwa na Marekani inatosha kukidhi mahitaji ya kujihami kwa sasa.Kiongozi huyo wa kijeshi anaongeza kuwa uwezekano wa kushambuliwa na nchi ya Iran ni mdogo sana.