1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow.Rais Putin akutana na Rais wa Angola Dos Santos.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxL

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa na mazungumzo hii leo pamoja na kiongozi mwenzake wa Angola Jose Eduardo dos Santos katika ikulu ya Urusi huko Kremlin mjini Moscow.

Mazungumzo yao yalituama juu ya namna ya kuimarisha mafungamano ya kiuchumi pamoja na nchi hiyo tajiri kwa almasi na mafuta barani Afrika.

Rais Vladimir Putin amesema.

”Nnaamini ziara yako itasaidia kuleta msukumo katika uhusiano wa nchi zetu mbili tukizingatia nyaraka kumi zilizotiwa saini hii leo zinazozungumzia ushirikiano katika sekta tofauti. Tunajuwa kwamba Angola ina neema kubwa ya kiuchumi na tunajua pia na hili ndio muhimu zaidi kwamba wananchi wa Angola wanaimani kubwa na Urusi. Tunaamini kwa hivyo huwo ni msingi muhimu wa kuendelezwa uhusiano wa pande mbili”.