MOSCOW: NATO na Urusi zitaendelea na majadiliano
27 Juni 2007Matangazo
Katibu Mkuu wa umoja wa kujihami wa mataifa ya magharibi,NATO,Jaap de Hoop Scheffer amekutana na Rais Vladimir Putin na waziri wa masuala ya nje wa Urussi,Sergei Lavrov mjini Moscow.Lakini yadhihirika kuwa hakufanikiwa hivyo kupunguza hali ya mvutano iliyopo hivi sasa,kati ya NATO na Moscow.Scheffer amemuambia Putin,hatua ya kuzuia mpango wa Umoja wa Mataifa kutoa uhuru kwa jimbo la Kosovo,huenda ikaathiri hali ya utulivu.Kwa upande mwingine,waziri Lavrov alisema,mipango ya Marekani ya kutaka kujenga mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora,nchini Jamhuri ya Czech na Poland huenda ikachafua kanda nzima.Hata hivyo,pande zote mbili zimekubali kuendelea na majadiliano, kwa azma ya kuondosha tofauti zilizopo kati ya pande hizo mbili.