1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Mgogoro wa nyuklia wa Iran utenzuliwe kwa mashauriano

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTv

Waziri wa masuala ya nje wa Urussi,Sergei Lavrov ametoa wito kwa Iran ionyeshe nia nzuri kuhusu mgogoro wa mradi wake wa kinyuklia.Alipokutana na mjumbe maalum wa Iran,Ali Akbar Welayati mjini Moscow,waziri Lavrov alisema,mzozo huo lazima utenzuliwe kwa njia ya mashauriano.Akaongezea kuwa msismamo wa Urussi haujabadilika.Kwa upande mwingine,Ali Akbar Welayati alisema,nchi yake inaunga mkono kikamilifu hatua ya Urussi kutafuta suluhisho la mgogoro huo.Desemba mwaka jana,Umoja wa Mataifa uliamua kuiwekea Iran vikwazo kadhaa kwa azma ya kuizuia nchi hiyo kurutubisha madini ya Uranium.Marekani inaituhumu Iran kuwa kwa siri,inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia.