1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Kinu cha kinuklia kitaanzakufanya kazi mwakani

27 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD8M

Urussi na Iran zimetia saini makubaliano yaliyopanga tarehe ya kuanzishwa kazi katika kiwanda cha kwanza cha nishati ya kinuklia,nchini Iran.Kiwanda cha Bushehr kinachojengwa na Urussi kusini-magharibi mwa Iran,kinatazamiwa kuwa tayari Septemba mwaka ujao na umeme unatazamiwa kupatikana mwezi wa Novemba.Nishati ya kinuklia lakini itakuwa tayari kwa matumizi mwezi wa Machi.Washington,imeishinikiza Moscow isitishe ujenzi wa kiwanda cha Bushehr kwa sababu ya hofu kuwa Iran huenda ikatumia ufundi wa kinuklia kutengeneza silaza za atomiki.