MOSCOW: Gorbachev apendekeza Kohl apewe Tuzo ya Amani
12 Juni 2007Matangazo
Mikhail Gorbachev aliekuwa rais wa Soviet Union ya zamani,amependekeza Kansela wa zamani wa Ujerumani,Helmut Kohl apewe Tuzo ya Amani ya Nobel.Gorbachev alieanzisha mfumo wa demokrasia nchini mwake katika miaka ya 80 ameandika barua kwa kamati ya Nobel mjini Oslo.Amesema,Kohl alichukua nafasi muhimu katika matokeo ya kihistoria yaliyokwenda kwa amani.Gorbachev binafsi alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1990.