1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco yaichapa Cameroon michuano ya CHAN

4 Februari 2021

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN Morocco watakuwa na fursa ya kulibeba tena kombe hilo watakaposhuka dimbani Jumapili katika fainali dhidi ya Mali mjini Yaounde, Cameroon.

https://p.dw.com/p/3os5t
Marokko Fußballmannschaft
Picha: picture-alliance/AA/J. Morchidi

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN Morocco watakuwa na fursa ya kulibeba tena kombe hilo watakaposhuka dimbani Jumapili katika fainali dhidi ya Mali mjini Yaounde, Cameroon. Soufiane Rahimi alifunga mabao mawili jana katika nusu fainali ya pili wakati Morocco walipowabomoa wenyeji Cameroon 4 - 0 mjini Limbe. Kama watashinda fainali hiyo, Morocco itaungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa washindi mara mbili wa mashindano hayo. Wakati Morocco ikipata ushindi rahisi, Mali ilitoka sare tasa baada ya muda wa ziada dhidi ya Guinea katika nusu fainali ya kwanza mjini Douala. Mali kisha ilipata ushindi kwa kufunga penalti 5 kwa 4. Mali pia waliwaondoa Congo Brazaville kupitia penalti katika robo fainali. Jumamosi, Cameroon watakana koo na Guinea katika mechi ya kumpata mshindi wa nafasi ya tatu.