1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco: Muungano tawala washindwa pakubwa katika uchaguzi

9 Septemba 2021

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Morocco yanaonyesha kuwa watawala wa muda mrefu nchini humo wameshindwa pakubwa.

https://p.dw.com/p/406ub
Marokko | Wahlen
Picha: Abdelhak Balhaki/REUTERS

Katika kikao na waandishi wa habari, waziri wa masuala ya ndani wa Morocco Abdelouafi Laftit amesema chama cha Haki na Maendeleo - Justice and Development, PJD, ambacho kilikuwa kinaongoza muungano uliokuwa unatawala kwa mwongo mmoja, kimeshuhudia uungwaji mkono wake bungeni kuporomoka kutoka viti 125 hadi viti 12 tu.

Mahasimu wake chama cha National Rally of Independents RNI kimenyakua viti 97 huku chama cha Authenticity and Modernity Party PAm kikipata viti 87 nacho chama cha Istiqlal kikiambulia viti 78 katika bunge lenye jumla ya viti 395.

Chama cha RNI ambacho kilikuwa chama kidogo katika muungano tawala, kinaongozwa na mfanyabiashara bilionea nchini humo Aziz Akhannouch.