Mogomo waitishwa Zimbabwe
9 Septemba 2007Matangazo
HARARE:
Shirikisho kuu la vyama vya wafanyikazi nchini Zimbabwe limeitisha mgomo wa siku 2 baadae mwezi huu ili kulalamika juu ya kusimasmishwa nyongeza za mishahara.
Wanachama 350.000 wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi la Zimbabwe Congress of Trade Unions wametakiwa kutokwenda makazini hapo septemba 19 na 20.
Wafanyikazi wamekasirishwa na kanuni ya rais Robert Mugabe ya August 30 inayopinga kuiongeza mishahara bila ruhusa ya serikali.