1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watoto wawili wauwawa Somalia

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVd

Miripuko kadhaa ilitikisa mji mkuu wa Somalia Mogadishu hapo jana na kuua watoto wawili pamoja na mzee mmoja.Watu wengine watano walijeruhiwa.Ghasia bado zinaikumba Somalia licha ya kuwepo juhudi za kuleta amani katika taifa hilo la Pembe ya Afrika lililosambaratika.

Bomu la kutegwa kando ya barabara liliripuka katika wilaya ya Gupta kaskazini mwa mji wa Mogadishu na kuwauwa kwa watoto hao wawili waliokuwa wakielekea shule.Katika tukio jingine wanamgambo walirusha magruneti dhidi wanajeshi wa Somalia na Ethiopia waliokuwa wakisaka sialaha kaskazini mwa wilaya ya Suqa-holaha na kujeruhi maafisa wawili.

Miripuko hii imetokea siku moja baada ya wanamgambo wanaungwa mkono na mahakama za kiislamu kuapa kuongeza nguvu mashambulio hadi pale wanajeshi wa Ethiopia watakapoondoka nchini Somalia.

Bado mazungumzo ya kutafuta maridhiano nchini humo yanaendelea huku wanamgambo wa mahakama za kiislamu na wazee wa ukoo mkubwa nchini humo wa Hawiye wakisusia vikao.