MOGADISHU:Wanajeshi wa serikali na Ethiopia waelekea Kismayo
31 Desemba 2006Matangazo
Wanajeshi wa serikali ya mpito wakisaidiwa na vifaru vya kijeshi vya Ethiopia wanasemekana kukaribia kuingia kwenye eneo linaloshikliwa na mahaka za kiislamu kusini mwa nchi.
Mji wa bandari wa Kismayu unasemekana kuwa mji wa mwisho unaoshikiliwa na mahakama za kiislamu baada ya kutimuliwa katika mji mkuu Mogadishu siku ya alhamisi kufuatia mapambano makali na vikosi vya Ethiopia.
Wakati huohuo kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu imesema mamia ya watu huenda wameuwawa kwenye mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia na kwamba maelfu yaw engine wamelazimika kukimbia makaazi yao.