MOGADISHU:Waandishi wawili wa habari wauawa Somalia
11 Agosti 2007Waandishi wawili wa habari wa radio nchini Somalia wameuawa leo hii katika matukio mawili tofauti
Katika tukio la kwanza Mahad Ahmed Elmi mwandishi wa habari wa kampuni ya HornAfrik Media inayomiliki vituo vya radio na televisheni aliuawa leo asubuhi wakati alipokuwa akienda kazini.
Mahad alipigwa risasi kadhaa na watu waliyokuwa na bastola ambapo mwili wake uliokotwa mita chache kutoka kwenye ofisi za kampuni hiyo ambayo ni ya binafsi.
Na mmiliki wa kampuni hiyo Ali Iman Sharmarke aliuawa na bomu la kutegwa ardhini wakati alipokuwa akirudi kutoka katika mazishi ya Mahad.
Afisa mmoja wa kampuni hiyo Farah Berey amesema kuwa mkuu wao aliuawa wakati alipokuwa akitoka katuka mazishi ya mwandishi wake na bomu lililotegwa ardhini.
Mji mkuu huo wa Somalia umekuwa katika hali mbaya ya usalama, pamoja na mkutano wa vikundi mbalimbali vinavyopingana kutangaza kusitisha makubaliano.Mkutano huo ulifanyika nchini Kenya wiki hii.