MOGADISHU:Rais wa shirikisho la Soka Somalia akabiliwa na tuhuma za ufisadi
26 Februari 2007Shirikisho la Soka duniani FIFA linamchunguza rais wa Shirikisho la soka nchini Somalia Muhyidin Hassan Ali baada ya kudaiwa kwamba ametumia vibaya maelfu ya dolla,fedha ambazo zililengwa kulipa mishahara ya wafanyikazi wa shirikisho hilo na madeni ya simu.
Kwa mujibu wa Afisa mmoja nchini Somalia rais huyo wa SFF alitoa kinyume cha sheria fedha zaidi ya dolla laki moja na kubakisha dolla 600 pekee katika akaunti.
FIFA imuandikia barua bwana Ali na kumtaka aeleze sababu za kutoa kitita hicho cha pesa.Kwa sasa bwana Muhyidin amesimamishwa kazi hadi Fifa itakakapokamilisha uchunguzi wake na kutoa uamuzi.
Kutoka na ukosefu wa serikali madhubuti nchini Somalia tangu kungolewa madarakani kwa Dikteta Siad Barre mwaka 1991 timu ya taifa ya Soka ya Somalia imekuwa ikifanya vibaya kabisa kutokana na ukosefu wa fedha na hali mbaya ya usalama.