Mogadishu:Maandamano kupinga jeshi la Ethiopia.
24 Julai 2006Matangazo
Watu 5,000 wameandamana nchini Somalia kupinga kuwepo kwa majeshi ya Ethiopia nchini mwao, maandamano ambayo yameitishwa na waislamu wanaolishikilia eneo la Somalia ya kusini.
Lengo hasa la maandamano hayo ni kushinikiza wanajeshi wa Ethiopia waondoke katika ardhi yao ambao wameingia huko Baidoa kwenda kuisaidia serikali ya muda isiyo na nguvu ya nchi hiyo.
Katika maandamano hayo huko Mogadishu kiongozi wa waislamu Sheikh Sharif Seikh Ahmed amesema, wanamgambo wanaweza kupambana na vikosi vya kijeshi vya Ethiopia lakini wanachokisubiri ni upatanisho wa kimataifa.