MOGADISHU:Kiongozi wa WFP Somalia akamatwa
17 Oktoba 2007Matangazo
Majeshi takriban 60 ya serikali yamevamia majengo ya Umoja wa mataifa hii leo na kumkamata na kumzuia mfanyikazi mmoja wa shirika la mpango wa chakula ulimwenguni WFP.
Chanzo cha kukamatwa kwa mfanyikazi huyo wa misadaa ambaye ni kiongozi wa shirika hilo mjini Mogadishu bado hakijulikani. Hata hivyo msemaji wa polisi anathibitihsa tukio hilo na hajaelezea sababu zake.
Ghasia zimesababisha mashirika mengi ya kutoa misaada kuondoka katika taifa hilo la pembe ya Afrika.