MOGADISHU:jeshi la Umoja wa Afrika lashambuliwa Somalia
18 Novemba 2007Matangazo
Waasi wanaoipinga serikali ya Somalia wamewashambulia askari wa jeshi la Umoja wa Afrika linalolinda amani nchini Somalia.
Waasi hao walikishambulia kituo cha majeshi ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu-Mogadishu.Muasi mmoja aliuawa baada ya majeshi ya Umoja huo kujibu shambulio.
Shambulio la waasi limefanyika siku mbili baada ya kiongozi wao Sheikh Aden Hashi Ayrow kuwaamrisha wapiganaji wake kulishambulia jeshi la Umoja wa Afrika.
Sehemu kubwa ya jeshi hilo ni la askari kutoka Uganda.