1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Ghasia zaongezeka tena nchini Somalia

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bl

Watu watatu waliuwawa mjini Mogadishu baada ya Wanajeshi wa Ethiopia hapo jana kuwashambulia kwa risasi waandamanaji wanaopinga kuwepo kwa wanajeshi hao katika ardhi ya Somalia.Maandamano hayo yametokea baada ya vikosi vya Ethiopia kufanya opresheni kali ya kuwasaka wanamgambo mjini Mogadishu waandamanji walichoma vituo viwili vya polisi.

Hatua hiyo imezusha upya ghasia nchini humo na kuzidisha hali ya wasi wasi.

Wakati huohuo maafisa wa serikali ya mpito wamewatolea mwito raia kuondoka katika eneo la kusini mwa Mogadishu ili kufungua njia ya kufanyika opresheni zaidi za kuwasaka wanamgambo.Ghasia hizi zinaongezeka huku bado kukiwa na mivutano kati ya rais Abdullahi Ahmed Yusuf na waziri mkuu Ali Mohammed Gedi.Rais Yusuf analitaka Bunge kumtimua kwenye wadhifa wake waziri mkuu Gedi.