1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Balozi mpya wa UN Somalia afanya ziara rasmi ya kwanza

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNW

Balozi mpya wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Ahmedou Ould Abdala anafanya ziara yake ya kwanza katika mji mkuu wa Somalia unaozongwa na vita ili kujadilia mahitaji ya kibinadamu ya nchi hiyo na maafisa wa ngazi za juu wa serikali.Maafisa hao wametoa wito wa kupata msaada ili kukabiliana na athari za mafuriko katika eneo la kusini mwa nchi hiyo aidha wakazi walioachw abila makao kufuatia vita mjini Mogadishu.

Hata hivyo mashirika ya misaada yanalalamika kuwa maafisa wa serikali ya Somalia wanatatiza shughuli zao.Balozi Abdala ambaye ni mwanadiplomasia kwa muda mrefu anayetokea nchi ya Mauritania alikabidhiwa wadhifa huo tarehe 12 mwezi huu.Kabla ya hapo alihudumu kwa miaka 5 kama mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa katika eneo la Afrika Magharibi