Mogadishu yaandaa michuano ya soka
24 Januari 2024Matangazo
Mji huo mkuu Mogadishu, ni mwenyeji wa mashindano hayo ya kwanza ya soka katika miongo mitatu.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuwavutia maelfu ya watu. Serikali ya Somalia kwa miaka mingi imefanya kazi ya kuurejesha kwenye hali nzuri uwanja huo wa taifa wa michezo wa mjini Mogadishu.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Somalia Ali Abdi Mohamed, amesema uwanja huo uliofanyiwa marekebisho unakusudiwa kutimiza madhumuni yake ya asili, ambayo ni kuandaa mechi za mpira wa miguu.
Maoni yake yameungwa mkono na waziri wa michezo wa Somalia, Mohamed Barre, ambaye amesema madhumuni ya uwanja huo ni kuwajumuisha watu wenye maslahi sawa ambao ni wapenzi wa soka.