1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wimbi jipya la wakimbizi Somalia

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ai

Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada,takriban watu 90,000 wameukimbia mji mkuu wa Somalia,Mogadishu ili kujiepusha na mapigano yaliyozuka kati ya wanamgambo wa Kiislamu na majeshi ya Somalia yanayosaidiwa na vikosi vya Ethiopia.

Mkurugenzi wa tawi la World Vision nchini Somalia amesema,wakimbizi hao hawana chakula wala maji. Mashirika ya misaada yanasema haya ni mapigano makali kabisa kupata kushuhudiwa,tangu miezi mitatu iliyopita.