MOGADISHU: Waziri Mkuu wa Somalia amejiuzulu
29 Oktoba 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Somalia,Ali Mohamed Gedi amejiuzulu,ikiwa ni siku chache baada ya kuzuka mapigano makali kabisa kati ya majeshi ya Ethiopia na wanamgambo wa Kiislamu mjini Mogadishu.
Gedi ametuhumiwa kuwa ameshindwa kudhibiti machafuko yanayosababishwa na wanamgambo wa Kiislamu katika mji mkuu wa Somalia.Vile vile, tangu miezi kadhaa kuna mvutano wa kisiasa kati ya Gedi na Rais Abdullahi Yusuf ambao hutoka koo tofauti.