MOGADISHU: Waziri mkuu wa Ethiopia azuru Somalia
6 Juni 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amezuru mji mkuu wa Mogadishu ma kufanya mazungumzo na rais wa mpito wa Somalia Abdullahi Yusuf pamoja na viongozi wengine.
Ziara ya waziri mkuu Meles Zenawi iliwekewa ulinzi mkali na aliondoka masaa machache baadae.
Hakuna habari zilizo tolewa kuhusu mazungumzo ya viongozi hao.