1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Wasomali waandamana kuyapinga majeshi ya Ethiopia.

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcg

Mamia ya Wasomali wameandamana katika mji mkuu Mogadishu dhidi ya kuwepo kwa majeshi ya Ethiopia na hatua ya kutaka watu kunyang’anywa silaha.

Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi, na watu walioshuhudia wamesema majeshi ya Ethiopia walifyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji.

Mtu mmoja anasemekana kuwa ameuwawa, na wengine kadha wamejeruhiwa.

Maandamano hayo yamekuja wakati serikali ya mpito imesitisha moja kwa moja mpango wa kuwanyang’anya silaha watu katika mji mkuu Mogadishu.

Muda wa mwisho uliopangwa hapo kabla kwa wakaazi wa Mogadishu kusalimisha silaha zao ulikuwa Alhamis, lakini watu wachache wameitikia wito huo.

Serikali ya mpito ya Somalia inataka kuweka udhibiti wake mjini Mogadishu baada ya kuwaondoa wanamgambo wa mahakama za Kiislamu wiki iliyopita kwa msaada wa Ethiopia.