MOGADISHU: Raia mmoja wa Somalia auwawa
25 Julai 2007Matangazo
Raia mmoja wa Somalia ameuwawa leo kwenye ufyatulianaji wa risasi mjini Mogadishu.
Mapambano hayo ya risasi yalianza baada ya mtu aliyekuwa amejifunika uso wake na aliyekuwa kwenye pikipiki kuwashambulia wanajeshi wa Ethiopia kwa grenedi wakati walipokuwa wakishika doria katika eneo la kusini mwa Mogadishu.
Sambamba na hayo watu tisa wamejeruhiwa baada ya kijana mmoja kuwashambulia polisi kwa grenedi kwenye soko la Bakara mjini Mogadishu hii leo.