MOGADISHU: Mkutano wa Somalia umeahirishwa tena
19 Julai 2007Matangazo
Mkutano wa upatanisho uliofunguliwa katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu umeahirishwa kwa mara nyingine tena.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mapambano makali kuzuka karibu na eneo kunakofanywa mkutano huo.Si chini ya watoto 6 wameuawa katika mashambulizi hayo mapya.
Meya wa jiji la Mogadishu,Mohamed Dheere amesema,kundi la wanamgambo wa Kiislamu liitwalo,“Shabab“ na magaidi ndio waliohusika na mashambulizi hayo. Akaongezea kuwa mashambulizi hayo yamekosea kulenga eneo la mkutano na badala yake watoto 6 waliokuwa wakicheza mpira karibu na hapo,wameuawa na wengine 3 wamejeruhiwa.