MOGADISHU: Mapigano mapya yazuka Somalia
4 Novemba 2007Matangazo
Mapigano makali yameripuka upya katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu.Ripoti zinasema mapigano hayo yametokea kusini ya Mogadishu na raia mmoja ameuawa.Mashahidi wanasema,Ethiopia imeimarisha vikosi vyake katika mji wa Mogadishu.Mwaka jana Ethiopia ilipeleka vikosi vyake kuisaidia serikali ya Somalia kuwatimua wanamgambo wa Kiislamu ambao kwa muda mfupi walidhibiti sehemu kubwa ya nchi.