MOGADISHU: Kituo cha polisi kimevamiwa Somalia
3 Agosti 2007Matangazo
Si chini ya watu 10 wameuawa katika mashambulizi yaliyozuka mji mkuu wa Somalia,Mogadishu ikishukiwa kuwa yamefanywa na waasi wa makundi ya Kiislamu.Katika shambulio moja peke yake,watu wasiopungua 9 waliuaw,baada ya kituo cha polisi kuvamiwa wakati wa usiku,kaskazini mwa Mogadishu. Mpita njia mmoja pia aliuawa,baada ya mshambulizi kurusha gruneti kwenye mkahawa unaotumiwa sana na maafisa wa kijeshi,kusini mwa Mogadishu.