1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Modi ajadili vita vya Ukraine na Kansela wa Austria

10 Julai 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anayeitembelea Austria amekutana na mwenyeji wake Kansela Karl Nehammer mjini Vienna leo, na kutoa mwito wa kutumika diplomasia katika kumaliza vita vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4i7b8
Narendra Modi na Alexander Van Der Bellen
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na mwenyeji wake Rais wa Austria Alexander Van Der BellenPicha: Heinz-Peter Bader/AP/picture alliance

Kwenye mazungumzo yao mjini Vienna, Kansela Nehammer amesema ilikuwa muhimu kukutana na Modi ili kuelewa msimamo wa India kwenye mzozo wa Ukraine na pia kumfahamisha mashaka ya Ulaya kuhusu mzozo huo.

Ziara ya Modinchini Austria, taifa mshirika wa Ukraine ambalo linazingatia sera ya kijeshi ya kutoegemea upande wowote, inafanyika siku moja baada ya kiongozi huyo wa India kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow. 

Soma pia:Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amwambia Putin kwamba vita sio suluhu

Modi, ambaye nchi yake nayo imejizuia kuchagua upande kwenye vita vya Ukraine,  amesema njia thabiti ya kuutanzua mzozo wa Ukraine ni kupitia mazungumzo, pendekezo ambalo limeungwa pia mkono na Austria.