1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnangagwa aiomba mahakama kutupilia mbali shauri la upinzani

15 Agosti 2018

Mawakili wanaomwakilisha Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wamewasilisha nyaraka za kuiomba Mahakama ya Kikatiba ya nchi hiyo kuitupilia mbali kesi ya upinzani ya kupinga ushindi wake.

https://p.dw.com/p/33CmR
Simbabwe Präsidentschaftswahl Emmerson Mnangagwa erklärter Wahlsieger
Picha: Getty Images/D. Kitwood

Mawakili wanaomwakilisha Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wamewasilisha nyaraka za kuiomba Mahakama ya Kikatiba ya nchi hiyo kuitupilia mbali kesi ya upinzani ya kupinga ushindi wake. Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imesema Mnangagwa na chama tawala cha ZANU-PF alishinda uchaguzi wa Julai 30 katika uchaguzi huo wa kwanza wa taifa hilo bila ya jina la aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kuwa kwenye karatasi ya kupigia kura. Tume ya uchaguzi ilisema Mnangagwa alipata asilimia 50.8 ya kura dhidi ya mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.3. Chama kikuu cha upinzani Movement for Democratoc Change- MDC Ijumaa iliyopita kiliwasilisha kesi mahakamani kikiitisha uichaguzi mpya au kiongozi wake Chamisa atangazwe kuwa mshindi. Mnangagwa aliifuta sherehe ya kuapishwa kwake iliyopaswa kufanyika Jumapili iliyopita kutokana na kesi hiyo iliofunguliwa na upinzani.