Mmisri kifungo miaka 15 kwa ujasusi
21 Aprili 2007Matangazo
CAIRO:
Mmisri alie na uraia wa Kanada amehukumiwa leo kifungo cha miaka 15 korokoroni kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Israel.Hakimu Sayyed al-Ghohari wa Mahkama kuu ya usalama mjini Cairo amemhukumu Mohammed Essam Ghoneim al-Attar,mwenye umri wa miaka 31 na waisraeli 3 walihukumiwa bila ya kuwapo mahkamani .
Mwanafunzi huyo wa zamani wa chuo kikuu cha Al Azhar,ametuhumiwa kulitumikia shirika la ujasusi la Isarel Mosad .Kwa muujibu wa mashtaka dhidi yake ,Attar aliwasiliana na waisrael hao nchini Uturuki ambako alianza kuwafanyia kazi za ujasusi kwa kutoa habari za waarabu wanaotumika huko ,mtindo ambao aliuendeleza alipohamia kanada.Attar hana haki ya kukata rufaa.