1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Mmarekani mwenye asili ya Kisaudi aachiwa huru Riyadh

21 Machi 2023

Raia wa Marekani aliyehukumiwa kwenda jela miaka 19 nchini Saudi Arabia baada ya kuwakosoa watawala wa Riyadh ameachiwa huru.

https://p.dw.com/p/4OyeZ
Saad Ibrahim Almadi
Picha: Ibrahim Almadi/AP/picture alliance

Saad Ibrahim Almadi mwenye umri wa miaka 72 Mmarekani mwenye asili ya Kisaudi alikamatwa mnamo mwaka 2021 baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kile ambacho mwanawe amekiita ujumbe mwepesi kuhusu masuala kadhaa ikiwemo vita nchini Yemen na mauaji ya mwaka 2018 ya mwandishi habari wa Kisaudi Jamal Khashoggi.

Almadi ameachiwa huru ghafla hii leo kwa mujibu wa mwanawe Ibrahim aliyezungumza na shirika la habari la AFP akiwa nchini Marekani. Hata hivyo Almadi pia anakabiliwa na marufuku ya kutosafiri iliyowekwa mwaka jana na hivyo basi hawezi kuondoka nchini Saudi Arabia.

Kesi ya Almadi imeuongeza mvutano kati ya  Riyadh  na Washington,washirika wa muda mrefu ambao hivi karibuni wameonesha kutofautiana kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo haki za binadamu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW