1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Mlipuko wauwa watu kadhaa katika fukwe mjini Mogadishu

3 Agosti 2024

Watu kadhaa wameuawa na wengine wamejeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa ulitokea kwenye fukwe maarufu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu jana jioni.

https://p.dw.com/p/4j4JW
Kijana akiruka kwenye maji ya Bahari ya India huko Hamarweyne, Mogadishu, Somalia
Kijana akiruka kwenye maji ya Bahari ya India huko Hamarweyne, Mogadishu, SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire, alieleza kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wakazi walipokuwa wakiogelea huko Liddo beach katika wilaya ya Abdiaziz, lakini hakutoa maelezo zaidi ya waliohusika na tukio hilo.

Soma pia: Al-Shabaab yashambulia kambi za jeshi Somalia na kuwaua watu 25

Ali Khaire alitoa salamu za rambirambi kwa familia na jamaa ya wale waliouawa katika mlipuko huo alioutaja kuwa shambulio la kigaidi ambalo limeendeshwa wakati kukiwa na msongamano wa watu, jambo alilosema linadhihirisha uadui wa wazi wa magaidi hao kwa watu wa Somalia.

Vyombo vya habari vya serikali ya Somalia vimesema vikosi vya usalama vimewakamata washambuliaji.