Mlipuko wauwa na kujeruhi askari wa NATO Afghanistan
21 Januari 2008Matangazo
KABUL:
Mlipuko,unaoaminiwa kuwa wa bomu umemuua mwanajeshi mmoja wa NATO na kuwajeruhi wengine kadhaa kusini mwa Afghanistan. Wanajeshi hao walikuwa katika ulinzi.Taarifa ya ushirika imesema kuwa mlipuko huo umetokea jana jumapili katika eneo lenye mashambulizi la kusini ambako mabomu ya barabarani yamekuwa yakitegwa na kulipuka kila mara. Hata hivyo NATO haikutoa wapi wanatoka wahanga wa shambulio hilo au mahali kulikotokea shambulio hilo.Lakini kwa upande mwingine NATO imesema wanajeshi waliojeruhiwa hali yao sio ya kutisha. Wanajeshi 10 wa vikosi vya ushirika wa NATO wameuawa nchini Afghanistan mwaka huu.