Mlipuko wa mgawaha wauwa watu 31 kaskazini magharibi China
22 Juni 2023Takribani watu 31 wamefariki katika mripuko wa gesi uliotokea kwenye mgahawa mmoja wa kuchoma nyama katika mji wa Yinchuan, kaskazini magharibi mwa China. Mkasa huo wa jana usiku umetokea katika kilele cha kuelekea tamasha la siku tatu la Dragon, ambako wakaazi wengi wa China hujumuika nje pamoja na marafiki.
Picha za video zilizorushwa na kituo cha utangazaji cha CCTV, zilionyesha maafisa kadhaa wa zimamoto wakipambana kukabiliana na moto wakati moshi mkubwa ukishuhudiwa kutokea ndani ya mgahawa. Watu tisa akiwemo mmiliki wa mgahawa, washika dau na mfanyakazi mmoja, wameshikiliwa na polisi kwa mujibu wa CCTV.
Rais wa China Xi Jinping ameagiza juhudi zaidi katika kuwatibu majeruhi na kuimarishwa kwa usimamizi wa usalama katika sekta muhimu ili kulinda maisha na mali za watu.