Mlipuko wa Beirut unatajwa kusababishwa na kemikali ya Ammonium Nitrate iliyohifadhiwa katika ghala moja bila kuzingatia masharti ya usalama. Je, ni tahadhari gani zinaweza kuchukuliwa kuepuka ajali kama hiyo?. Swali hilo linajibiwa na Justin Ngaille, Mkurugenzi wa Udhibiti na Matumizi salama ya Mionzi kutoka Tume ya Atomik ya Tanzania.