1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mladic sasa afikishwa The Hague

1 Juni 2011

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, wameikaribisha hatua ya kumhamishia Ratko Mladic The Hague kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

https://p.dw.com/p/11S5F
Helikopta ya jeshi la Polisi la Uholanzi inayoaminiwa kumchukua Ratko Mladic
Helikopta ya jeshi la Polisi la Uholanzi inayoaminiwa kumchukua Ratko MladicPicha: dapd

Msemaji wa mahakama hiyo amesema Mladic, ambaye awali alichelewesha kuhamishwa kwake kwa sababu za kitabibu, atafanyiwa uchunguzi mwengine kamili wa afya yake na kisha kuwekwa katika mahabusu maalumu kwa siku chache za kwanza.

Jenerali huyo wa zamani wa jeshi la Serbia-Bosnia anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari na anatuhumiwa kwa kupanga mauaji ya kikatili ya Waislamu 8,000 huko Srebrenica mnamo mwaka 1995.

Pia anashtakiwa kwa kuuzingira mji wa Sarajevo kwa miezi 44 ambapo watu 10,000 waliuwawa. Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwishoni mwa wiki hii.

Mwandishi: Bruce Amani/ZPR
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman